Miso-Kare® (MISOPROSTOL 200mcg)

Miso-Kare® (MISOPROSTOL 200mcg)

Vidonge vya MISO-KARE vina 200mcg ya Misoprostol, analogi ya prostaglandini E1 (PGE 1).

Misoprostol ni ya kundi la homoni zinazoitwa prostaglandins ambazo zinaweza kusababisha mikazo ya uterasi na kufungua mlango wa kizazi (cervix). Ingawa prostaglandini ni nzuri sana, ufanisi wake unategemea idadi ya vipokezi vya prostaglandini kwenye uterasi na hii inatofautiana kulingana na ikiwa mwanamke ni mjamzito na yuko katika hatua gani ya ujauzito.

Miso-Kare® (MISOPROSTOL 200mcg)


Mwishoni mwa ujauzito: kuna vipokezi vingi na dozi ndogo ya misoprostol husababisha mikazo yenye nguvu. Uangalifu maalum unahitajika kwa wanawake ambao mimba imetungwa nje ya kizazi. Haitumiwi na wanawake ambao wamewahi kujifungua kwa njia ya upasuaji (caesarean sections) inaweza kusababisha kuchanika kwa mashono katika uterasi. Mipasuko ya uterasi pia imeripotiwa mara kwa mara katika uterasi isiyona kovu

Katika mimba iliyo changa: kuna vipokezi vichache na dozi kubwa za misoprostol zinaweza kuhitajika kutolewa mara kwa mara ili kuleta athari (kutoa matokeo tarajiwa). Hakuna matatizo yaliyoripotiwa katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na kwa wanawake ambao wamewahi kujifungua kwa njia ya upasuaji (caesarean sections).

Pharmacokinetics

Misoprostol hufyonzwa kwa urahisi na hupitia mmeng’enyo ili kupata asidi yake, hufungamana na plasma protini. na matokeo ya kumeng’enywa kwake ni pamoja na analogi za prostaglandin F. Mchanganyiko huu hutokea dawa inayojulikana kama lipophilic methyl ester pro na hubadilishwa kwa urahisi kuwa asidi, ambayo inafanya kazi kibiolojia ndani ya mwili. Baada ya kumeza kidonge kwa mdomo, kilele cha dawa kwenye damu (plasma) hufikiwa ndani ya dakika 30 na hupungua haraka kwa dakika 120. 80% ya dawa hutolewa kwa njia ya figo na 15% kupitia kinyesi

Matumizi

Kwa matibabu ya

  • Kutokwa na damu baada ya kujifungua
  • Tiba baada ya utoaji mimba

Maonyo na tahadhari

Mgonjwa anaweza kuhitaji matibabu ya haraka kwa maumivu na mfadhaiko wa tumbo (gastric irritation) baada ya kumeza Misoprostol. Pia mgonjwa anapaswa kupewa maagizo juu ya nini cha kufanya ikiwa mfadhaiko wa tumbo (gastric irritation), kutokwa na damu nyingi au athari nyingine mbaya itatokea. 

Kifaa cha Ndani ya Uterine, ambacho hutumika kama uzazi wa mpango kuzuia mimba kutungwa, (IUD) kinapaswa kuondolewa kabla ya matibabu ya misoprostol. Wagonjwa ambao wana ujauzito unaoendelea wakati wa ziara ya mwisho wana hatari ya uharibifu wa fetusi kutokana na matibabu. Oxytocin haipaswi kutumiwa baada ya masaa 6 ya kutumia dozi ya mwisho ya misoprostol. Kunaweza kuwa na hatari ya kuongezeka kwa tachysystole ya uterasi (uterine tachysystole), kuchanika kwa uterasi, meconium passage, meconium staining of amniotic fluid na kujifungua kwa upasuaji kutokana na msisimko mkubwa wa uterasi kama utatumia dozi kubwa ya Misoprostol.

Hairuhusiwi kutumika

Misoprostol imekataliwa ikiwa mgonjwa anayo

  • Hypersensitivity kwa prostaglandini (Allergy)
  • Ujauzito uliothibitishwa au unaoshukiwa kuwa nje ya kizazi au wingi wa adnexal ambao haujatambuliwa
  • Kama anatumia Kifaa cha Ndani ya Uterine (IUD) kwa ajili ya uzazi wa mpango
  • Kushindwa kwa adrenal ya muda mrefu (Chronic adrenal failure)
  • Matatizo ya kutokwa sana na damu  au upo katika tiba ya dawa za kufanya damu isiendelee kutoka, kutibu bleeding (anticoagulants)
  • Porphyria ya kurithi
  • Kukomaa kwa kizazi

Athari mbaya

  • Mgonjwa anaweza kupata maumivu kutokana na mikazo ya uterasi
  • Kutokwa na damu nyingi sehemu za siri
  • Mshtuko
  • Maumivu ya nyonga
  • Kupasuka kwa uterasi
  • Madhara ya njia ya utumbo kama vile kuhara, maumivu ya tumbo, kichefuchefu, gesi tumboni, dyspepsia, maumivu ya kichwa, kutapika na kuvimbiwa, kutetemeka, kizunguzungu.

Mwingiliano dawa nyingine

Misoprostol haiingiliani na athari za manufaa za aspirini kwenye ishara na dalili za arthritis ya baridi yabisi. Misoprostool haina madhara makubwa kwenye viwango vya damu na athari za antiplatelet kwa mgonjwa ambaye yupo kwenye matibabu ya aspirini. Misoprostol haina athari kubwa kwenye kinetics ya diclofenac au ibuprofen. Madhara ya kawaida ya Misoprostol ni kuhara na maumivu ya tumbo. Madhara haya yanaweza kuongezeka ikiwa misoprostol itatumika wakati huo huo na antacids (dawa za kupunguza acid tumboni).

Kipimo (dosage) na namna ya kutumia

600mcg imezwe kwa njia ya mdomo kwa ajili ya matibabu ya kutokwa na damu baada ya kujifungua na tiba baada ya mimba kutoka.

Kuzidisha kipimo

Dalili za ovedosage ya misoprostol (kutumia kiwango kikubwa) hazijulikani vyema lakini zinaweza kujumuisha mfadhaiko wa tumbo, maumivu ya tumbo, kuhara, kusinzia, kutetemeka, kifafa, ugumu wa kupumua, homa, shinikizo la chini la damu na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.

MANENO MUHIMU

  • matumizi ya misoprostol 200 mg
  • miso kidonge jinsi ya kutumia
  • miso kare tablet anatumia
  • madhara ya misoprostol kwa utoaji mimba
  • jinsi ya kutumia misoprostol ukeni
  • madhara ya misoprostol ukeni

VIUNGO

Post a Comment

0 Comments