Je kunamadhara yoyote iwapo hutashiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu?

 Je kunamadhara yoyote iwapo hutashiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu?

Katika maisha ya kila siku ni jambo la kawaida kwa mtu yeyote ambaye ameshafikia umri wa balehe kufikiria au hata kushiriki tendo la ndoa. Katika jamii nyingi, kushiriki tendo hili imehalalishwa kwa ajili ya wanandoa pekee na hujulikana kama tendo la ndoa. Tendo hili pia hufanywa kwa ajili ya kujiburudisha kama starehe, kwa watu wa umri tofauti tofauti na hujulikana pia kama kufanya mapenzi. Lakini, Je kuna madhara yoyote kama mtu hatashiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu?

Kiwango cha kushiriki tendo la ndoa hutofautiana kati ya mtu na mtu na pia hutofautiana kulingana na umri. Hakuna kiwango maalumu ambacho kinatambulika kuwa ni kiwango sahihi cha kushiriki tendo la ndoa au mara ngapi inatakiiwa mtu ashiriki kwa wiki au kwa siku. Tafiti zinabainisha kwamba, iwapo mtu hatashiriki mapenzi kwa miezi kadhaa au miaka, ananafasi kubwa ya kutokuona mabadiliko yoyote mabaya kiafya.

couple having sex
Photo by ROMAN ODINTSOV from Pexels


Tafiti pia zinabainisha kwamba kushiriki mapenzi mara kwa mara kuna faida kiafya kama vile kuimarisha kinga ya mwili, kupunguza shinikizo laa juu la damu, kupunguza mfadhaiko, na kupunguza hatari za kupata magonjwa ya moyo.

Baadhi ya faida hizi kama vile kupunguza mfadhaiko huweza kupatikana kwa kujichua (masturbation).

Kwa wanaaume, afya ya tezi huimarika kwa kuejaculate mara kwa mara. Utafiti uliofanyika mwaka 2016 uligundua kwamba kwa wanaume ambao hu ejaculate angalau mara 21 kwa mwezi wananafasi chache sana kupata saratani ya tezi kulinganisha na wale ambao wana ejaculate mara 4-7 kwa mwezi. Utafiti huu ulifanywa na Jennifer R. Rider, Kathryn M. Wilson na washirika, ulichapishwa tarehe 28 March 2016 katika jarida linalojulikana kama The Journal of European Eurology.

Kwa wanawake, kushiriki mapenzi mara kwa mara kuimarisha misuli ya nyonga ambayo hushikiria kibofu, kuimarisha kazi ya kibofu na kupunguza athari za kushindwa kuzuia mkojo (urinary incontinence and leakage)

Je kuna faida zozote za kufanya mapenzi/tendo la ndoa?

Kufanya mapenzi kuna faida kadhaa kwa afya ya mwili na akili. Hizi ni baadhi ya ffaaida za kufanya mapenzi

·         Kupunguza stress/mfadhaiko: Kufanya mapenzi husababisha mwili kutoa homoni kama vile oxytocin na endorphins, ambayo husaidia kupunguza mfadhaiko na kuboresha ustawi wa kihisia.

·         Kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo: Kufanya mapenzi kuna faida za kiafya kama vile kupunguza shinikizo la damu na kuboresha mtiririko wa damu, jambo ambalo linaweza kupunguza hatari ya kupata shinikizo la juu la damu.

·         Kupunguza maumivu: Kufaanya mapenzi husaidia kuuachiliaa homoni za kuzuia maumivu kama vile endorphins, ambazo hupunguza maaumivu na kufanya ujihhisi vizuri.

·         Kuboresha usingizi: Kufanya mapenzi husaidia kupunguza mkusanyiko wa homoni za mfadhaiko mwilini na hivyo kukufanya kupata usingizi bora.

·         Kuimarisha kinga ya mwili: Kufanya mapenzi husaidia kuimarisha kinga ya mwili kwa kusababishaa kuzalishwa kwa kemikali ambazo husaidia kuondoa dalili zitokanazo na maambuziki ya vimelewa wasababishao magonjwa hasa virusi.

·         Kuboresha afya ya akili: Kufanya mapenzi husaidia kuondoa dalili za unyongovu, kupunguza wasiwasi na kuboresha hisia za furaha.

Kufanya maapenzi inatakiwa kuwa kwa hiari na kwa usalama ili kuffurahia faida hizi.

Athari za kutofanya mapenzi

Ni kawaida kwa watu kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuwa mbali na mwenzi wako, kukosa maelewano katika mahusiano, matatizo ya kiafya au sababu nyinginezo. Hata hivyo hali ya kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu inaweza kuathiri afya ya akili.

·         Mfadhaiko: Kutofanya mapenzi kunaweza kusababisha mkusanyiko wa homoni za mfadhaiko. Hali hii huweza kupelekea kuwa na wasiwasi, kukosa ujasiri wa kufaanya tendo la ndoa kwa ufanisi na mfadhaiko

·         Kukosa usingizi: Kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kupunguza mkusanyiko wa homoni zza mfadhaiko mwilini na kusaidia kupata usingizi bora. Kukosa usingizi kunaweza kusababisha uchovu na kusababisha matatizo ya afya ya akili na mwili.

·         Kuongezeka kwa hatari yaa magonjwa: Kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kuimarisha kinga ya mwili. Kutofanya mapenzi kunaweza kuongeza hatari ya kuugua magonjwa kama vile shinikizo la damu, magonjwa ya akili, na magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili.

·         Kuongezeka kwa hatari ya kiharusi: Kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kupunguza shinikizo la damu na kuboresha mtiririko wa damu. Kutofanya mapenzi kuunaweza kuongeza hatari ya kiharusi

·         Kupungua  kwa hamu ya kufanya mapenzi; Kama mtu hajafanya mapenzi kwa muda mrefu anaweza kupoteza hamu ya kufanya mapenzi na kuwa na uwezekano mkubwa wa kutohitaji tena tendo la ndoa. Hii inaweza kuathiri maisha ya mahusiano na mwenzi wako.

·         Msongo wa mawazo: Kutokana na kushindwa kutekeleza haja ya kijinsia, mtu anaweza kukumbwa na msongo wa mawazo na huzuni.

·         Matatizo ya kiafya: Kutokana na kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu, mtu anaweza kuwa na hatari ya kupata matatizo yaa kiafya kama vile matatizo ya kushindwa kusimamisha uume (erectile dysfunction) au matatizo ya kizazi kwa wanawake.

 

 

                                                                                                            

 

Post a Comment

0 Comments