Aina mbalimbali za minyoo na dawa za kutibu minyoo
Minyoo ni wadudu ambao huingia ndani ya mwili wa mwa mtu kupitia vyanzo mbalimbali kama vile kula chakula ambacho hakijapikwa vizuri au kuandaliwa katika mazingira ya usafi au hata kupitia maji, matunda na mbogamboga. Minyoo wapo katika kundi la wanyama, wana seli mbalimbali (multicellular). Minyoo wamegawanyika katika makundi matatu ambayo ni Nematodes, Trematode na Cestode.
Minyoo katika makundi haya wanasifa tofauti, maumbo tofauti kwa kila kundi na miundoo yao ya mwili ipo tofauti pia. Tofauti hizi ndizo ambazo huamua ni aina gani ya dawa inafaa kutumika ili kutibu minyoo kwa mgonjwa. Hivyo ni muhimu kabla ya kuanza kutumia dawa ya minyoo, kufahamu ni aina gani ya minyoo ambayo imegundulika kupitiia vipimo vya maabara.
Katika makundi haya ya minyoo pia huathiri sehemu tofauti za mwili. Minyoo inaweza kusafiri mpaka kwenye ubongo na kusababisha athari, minyoo pia huweza kuathiri mishipa ya moyo, mapafu na macho.
Minyoo pia huweza kutoka nje ya ukuta wa tumbo na kusafiri mpaka kwenye ngozi na kusababisha muwasho wa ngozi na vipele. Katika mfumo wa upumuaji minyoo huweza kupelekea mgonjwa kukohoa mara kwa mara. Minyoo pia huweza kupelekea mgonjwa kuwa na upungufu wa damu.
Vyanzo vya minyoo kwa mtu
• Udongo wenye minyoo (Geo-helminthes), waji (cercariae blood flukes) na chakula (Taenia kupitia nyama ambayo haijapikwa vizuri)
• Wadudu ambao hufyonza damu (filarial worms)
• Wanyama wafungwao au wa porini amabo wameathirika (echinococcus katika mbwa)
• Kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine (Enterobius vermicularis, Hymenolopis nana)
Minyoo pia huweza kuingia mwilini kupitia milango ya fahamu kama vile mdomo, ngozi na njia ya upumuaji kwa kuvuta hewa yenye mayai ya minyoo.
Trematodes
Minyoo hii ipo katika familia ya phylum platyhelminthes. Minyoo hii wanapatikana katika mazingira tofauti. Kwa wanayama wenye uti wa mgongo, minyoo hii hupatikana katika utumbo, kwenye ini, kibofu, kongosho, na mrija unaosafirisha mkojo kutoka kwenye figo kuelekea kwenye kibofu.
Minyoo wanaosababisha kichocho wapo katika kundi hili. Minyoo hawa wa kichocho kujulika kwa majina tofauti kulingana na mahala ambapo huathiri mwilini.
• Schistosoma mansoni: Minyoo hawa hushambulia itumbo mwembamba wa chakula
• Schistosoma haematobium: husababisha kichocho katika njia ya mkojo
• Schistosoma japonicum: husababisha kichocho cha uutumbo mwembamba
• Schistosoma intercalatum: husababisha kichocho cha utumbo mwembamba
• Schistosoma mekongi: husababisha kichocho katika utumboo mwembamba. Huathiri sana wanyama tofauti na binadamu.
Dalili na malalamiko
Mgonjwa mwenye kichocho anaweza kuonyesha dalili na malalamiko kama vile; upungufu wa damu na maumivu makali wakati wa kukojoa. Vimbe katika kibofu cha mkojo na ini na kongosho kuvimba.
Muwasho wa ngozi, kujisaidia choo kilicho changanyika na damu na kuvimba kwa ini na kongosho hutokea katika maambukizi ya S. mansoni.
Minyoo S. haematobium huweza kusababisha saratani ya kibofu.
Kichocho hutibiwa na dawa ijulikanayo kwa jina la Plaziquantel kwa kipimo cha 40mg/kg kwa dozi mbili tofauti.
Nematodes (Minyoo mviringo)
Hawa wapo katika familia ya minyoo ijulikanayo kama Phylum Nemathelminthes (Aschelminthes). Minyoo katika kundi hili ni pamoja na:
Minyoo inayo athiri utumbo mwembamba
• Ascaris lumbricoides
• Hookworms
• Strongyloides stercoralis
• Enterobius vermicularis
• Trichuris trichuira
Minyoo ambayo hukaa kwenye damu na tishu za mwili
• Filarial worms
• Dracunculus medinensis
• Trichinella
• Larva migrans
Ascaris lumbricoides hutaga mayai yao na kutotoa kweenye sehemu ya utumbo mwembamba (duodenum). Lava hupenya ukuta wa tumbo na kuingia kwenye mzunguko wa damu kwenda kwenye moyo hadi kwenye mapafu. Kutoka kwenye mapafu hushuka kurudi kwenye utumbo mwembamba ambapo huwa wakubwa. Minyoo wakike hutaga mayai kwenye udongo na hukomaa ndani ya wiki 2.
Mgonjwa mwenye aina hii ya minyoo hulalamika maumivu ya tumbo. Kwenye mapafu husababisha vimbe (Loeffler’s syndrome) na dalili za nimonia.
Mgonjwa anaweza kulalamika muwasho kuzunguka eneo la kutolea kinyesi (mkundu). Wakati wa usiku eno hilo huwasha na kuchoma choma mithili ya kuchomwa sindano. Minyoo pia huweza kusababisha appendix kuvimba na kusababisha appendicitis.
Dawa zinazoweza kutumika dhidi ya minyoo hawa ni pamoja na Mebendazole, Albendazole na Piperazine.
Hookworms: Dawa dhidi ya minyoo hawa ni pamoja na Mebendazole, na Thiabendazole ambayo hupakaa kwenye ngozi.
Strongyloides stercoralis: Mgonjwa hujisaidia choo chenye kamasi. Minyoo amabao wameathiri mapafu, mgonjwa huwa na dalili za nimonia. Dawa dhidi ya minyoo hii ni Thiabendazole 25mg/kg. Kila baada ya masaa 12 kwa muda wa siku 3.
Trichuris trichiura: Mgonjwa hujisaidia choo kilichochanganyika na damu na kamasi. Mebendazole hutumika dhidi ya minyoo hawa.
Wuchereria bancrofti: Minyoo hawa huingia mwilini kama utang’atwa na mnyama au mdudu aliye athirika. Mgonjwa huvimba tezi za miguuni na tezi za ukeni.
Tezi zilizovimba husababisha ugonjwa ujulikanao kama Elephantiasis, mguu wa tembo na busha.
Diethyl carbamazine (DEC). 2mg/kg kila baada ya masaa 8 kwa muda wa wiki 2 ni dawa ambayo hutumika dhidi ya minyoo hawa.
Onchocerca volvulus: Minyoo hawa husababisha upofu, ugonjwa ujulikanano kama Onchocerciasis au river blindness. Mgonjwa hubadilika rangi ya ngozi, ngozi huvimba na kuwa kama ngozi ya mjusi au kenge (huwa na magamba).
Busha (Elephantiasis) katika sehemu za siri na upofu.
Ivermectin 50mg/kg ambayo hutolewa kila baada ya miezi 6 au 12 hutumika dhidi ya minyoo hii. Matibabu huweza kuchukua zaidi ya mwaka kukamilika.
Je utajikingaje dhidi ya minyoo?
• Tumia maji safi na salama katika vyoo
• Epuka kukojoa ama kujisaidia choo katika mapori, mifereji ya maji na madimbwi
• Safisha mazingira yako na kuondoa mazalia ya konokono
• Matumizi ya viwatilifu katika madimbwi na mifereji ili kuua konokono
• Kuosha matunda na mbogamboga kwa maji safi tiririka na salama
• Kuandaa chakula katika mazingira safi na salama
• Kula nyama iliyopikwa kikamilifu
• Kuosha mikono kwa sabuni na maji tiririka kabla ya kula chakula, matunda na mboga.
0 Comments